• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Newala Town Council
Newala Town Council

Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano ya Umma
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi, Maliasili na Mipango Miji
      • Kazi
      • Usafi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Video
    • Maktaba ya picha

Idara ya elimu sekondari Halmashauri ya ya Mji Newala imepokea vitabu 8150 vya masomo ya sanaa na sayansi kutoka TAMISEMI

Posted on: May 25th, 2022

Idara ya elimu sekondari halmashauri ya ya Mji Newala imepokea vitabu 8150 vya masomo ya sanaa na sayansi ikiwa awamu ya pili mgao wa vitabu kutoka wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Akiongea mara baada yakupokea vitabu hivyo na kuvigawa kwa wakuu shule Mei 25, 2022 Mkuu wa idara ya elimu sekondari halmashauri hiyo Mwl. Athuman Salum ameishukuru serikali kwa kutekeleza kwa vitendo utoaji wa rudhuku ya uendeshaji ya 50% ambayo serikali iliahidi kuwa itaelekeza kwenye usambazi ya vifaa vya kufundishia shuleni.

Hata hivyo Mwl. Salum amewataka wakuu wa shule kuvigawa vitabu hivyo kwa walimu wa wasomo ili wanafunzi wavitumie kwa kujisomea na kuongeza ufaulu kwenye mitihani yao kwa kuwa serikali imetekeleza wajibu wake na jambo lililobaki ni wanafunzi kunufaika.

Aidha Mkuu huyo amefafanua kuwa vitabu nilivyopokelewa ni vya masomo ya Fizikia, Jografia, Hesabu, Kemia, Baiolojia, Uraia pamoja na Kiswahili ambavyo kwa masomo ya sayansi zinaenda kupunguza uhaba wa vitabu kwa wastani wa kitabu kimoja kwa wanafunzi 2 na kwa masomo ya sanaa wastani wa kitabu kimoja kwa watoto 4 tofuti na hapo awali ambao ilikua kitabu kimoja kwa watoto 6.

Akiongea kwa niaba ya wakuu wa shule waliopokea vitabu hivyo Mkuu wa shule ya sekondari Newala Mwl. Briton Limbe, amesema vitabu hivyo vinakwenda kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitabu shuleni baada ya kubalika kwa mtaala, shule zilikosa vitabu na walimu kwa uapande mwingine walilazimika kutumia njia za TEHAMA kuvitafuta mtandaoni.

Mwl. Limbe amewataka wanafunzi kuchukua hatua za maksudi katika kuongeza juhudi kwenye kujifunza na kujisomea kwa kuwa serikili inatekeleza jambo hilo huku ikimlenga mwanafunzi katika kumuandalia mazingira bora ya wao ya kupata elimu.



Matangazo

  • TANGAZO NAFASI YA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI January 25, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III April 14, 2023
  • WITO WA MAFUNZO YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA BVR OPERATORS JIMBO LA NEWALA January 21, 2025
  • WALIOCHAGULIWA KUWA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA BVR OPERATORS JIMBO LA NEWALA MJINI January 14, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Bilioni 21.5 baji ya Mji Newala 2023/2024

    August 04, 2023
  • Tupo nanenane kutoa elimu kwa wananchi itakayobadilisha mitazamo yao kwenye kilimo.

    August 02, 2023
  • Serikali imesema wanawake na vijana wanaweza kukuza kilimo biashara na kuwa endelevu

    August 01, 2023
  • Mkuu wa mkoa Mtwara aridhishwa na utekelezaji wa miradi ya BOOST na ujenzi wa mabweni

    July 29, 2023
  • Tazama zote

Video

Video nyingine

Kurasa za Haraka

  • Sanitation day
  • Tender
  • Uhuru torch

Kurasa Mashuhuri

  • Higher Education Students' Loans Board
  • National Examinations Council of Tanzania
  • Tanzania National Electoral Commission
  • PSPF Pension Fund
  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration and Local Government

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Newala-Mtwara

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 39

    Simu: (+255) 023 2935398

    Mobile: PS (0684439199)

    Barua pepe: info@newalatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Disclaimer
    • Sera ya Faragha
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya eneo la tukio
    • Huduma

Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa