• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Newala Town Council
Newala Town Council

Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano ya Umma
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi, Maliasili na Mipango Miji
      • Kazi
      • Usafi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Video
    • Maktaba ya picha

Mwenge wa Uhuru imerishwa na miradi yote Halmashauri ya Mji Newala na kuhimiza uzalendo

Posted on: April 8th, 2023

Wilaya ya Newala imepokea Mwenge wa Uhuru 2023 katika kijiji cha Lidumbe Halmashauri ya Mji Newala kwa ajili ya kuanza kufanya shughuli za kukagua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi, kuona na kufungua miradi ya maendeleo.

Akipokea Mwenge huo Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaj Mwangi Rajabu Kundya Alhamisi Tarehe 6 Aprili, 2023 kutoka kwa Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe. Patrick Sawala, alisema wilaya ya Newala ina miradi 16 ya maendeleo katika halmashauri zake mbili yenye thamani ya shilingi bilioni 5.82 na utakimbizwa umbali wa kilomita 166.

Aidha Mwenge ukiwa Halmashauri ya Mji Newala umepitia miradi 9 na kuridhishwa na miradi yote ikiwemo ikiwemo kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Mnaida unaohusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 225,000 na miundombinu ya usambazaji maji utakaowanufaisha watu 20,547 wa Kata za Mcholi 1 na 2 pamoja na Kata ya Mtumachi wenye thamani ya shilingi bilioni 2.326.

Aidha mbio hizo zimezindua nyumba ya mtumishi wa Zahanati ya Mnaida iliyojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kutumia force account yenye thamani ya shilingi milioni 52.452 ambapo kati ya fedha hizo shilingi laki 5 ni mchango wa nguvu za wananchi.

Kufuatia kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023 isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”  Halamshauri ya Mji Newala kwa kushirikiana na TFS iliunda kuunda klabu ya uhifadhi mazingira shuleni na kuandaa maradi wa upandaji miti 775 yenye thamani ya shilingi milioni 1.212.

Aidha katika kuendelea kusimamia wa kauli mbi hiyo Halmashauri ilikua na maradi wa kikundi cha wajasiriamali wanaojihusisha na ukusanyaji na uchakataji wa plastiki chakavu kilichowezeshwa na halmashauri kununua mashine kupitia mikopo ya 10% wenye thamabani ya shilingi milioni 8, kwa leng kukabiliana na changamoto ya usafi wa mazingira pamoja na  kuwapatia kipato.

Miradi mingine iliyopitiwa Mwenye wa Uhuru Halmashauri ya Mji Newala ni Ujenzi wa barabara ya lami ya Chitandi yenye urefu wa kilometa 2 yenye thamani ya shilingi milioni 975, Mradi wa kufungua huduma kituo cha Afya Mnekachi, Mradi ya klabu ya kupinga rushwa shule ya sekondari Makondeko pamoja na ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mtangalanga yenye thamani ya shilingi milioni 40.

Aidha ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru umewasisitiza wananchi kuwa wazalendo wa Taifa na kuzingatia utunzaji mazingira ili kuondoka na hali mbaya ya mabadiliko ya tabia ya nchi, kuzingatia lishe bora, kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, kujikinga dhidi ya malaria, kupinga rushwa na kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mwenye wa Uhuru 2023, Halashauri ya Mji Newala umekimbizwa umbali wa kilometa 88 katika Tarafa 2, Kata 12, Mitaa3  na Vijiji 20  kisha kukabidhiwa halmashauri ya wilaya Newala.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI YA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI January 25, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III April 14, 2023
  • WITO WA MAFUNZO YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA BVR OPERATORS JIMBO LA NEWALA January 21, 2025
  • WALIOCHAGULIWA KUWA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA BVR OPERATORS JIMBO LA NEWALA MJINI January 14, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Bilioni 21.5 baji ya Mji Newala 2023/2024

    August 04, 2023
  • Tupo nanenane kutoa elimu kwa wananchi itakayobadilisha mitazamo yao kwenye kilimo.

    August 02, 2023
  • Serikali imesema wanawake na vijana wanaweza kukuza kilimo biashara na kuwa endelevu

    August 01, 2023
  • Mkuu wa mkoa Mtwara aridhishwa na utekelezaji wa miradi ya BOOST na ujenzi wa mabweni

    July 29, 2023
  • Tazama zote

Video

Video nyingine

Kurasa za Haraka

  • Sanitation day
  • Tender
  • Uhuru torch

Kurasa Mashuhuri

  • Higher Education Students' Loans Board
  • National Examinations Council of Tanzania
  • Tanzania National Electoral Commission
  • PSPF Pension Fund
  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration and Local Government

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Newala-Mtwara

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 39

    Simu: (+255) 023 2935398

    Mobile: PS (0684439199)

    Barua pepe: info@newalatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Disclaimer
    • Sera ya Faragha
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya eneo la tukio
    • Huduma

Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa